Mo Dewji Foundation donates 4 tonnes of food to 350 families

Taasisi ya Mo Dewji Foundation kwa kushirikiana na Volunteer in Development Foundation imetoa msaada wa vyakula kwa Watoto 690 kwa ajili ya mfungo wa Ramadhan.

Msaada huu ni sehemu ya malengo ya Taasisi kurudisha kwenye jamii katika kipindi hiki ambapo inatekelezwa ibada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Watoto hawa wanatoka kwenye vituo vya Watoto ya yatima pamoja na kaya maskini katika mikoa ya Dar es Salaam na Pemba.

Bidhaa zilizotolewa ni pamoja na mafuta ya kupikia, unga wa ngano, unga wa sembe na tambi pakti za tambi, vyote ambavyo vina thamani ya zaidi ya Milioni 9. Zoezi la ugawaji wa bidhaa hizo kwa Watoto hao litasimamiwa na Taasisi ya Volunteer in Development Foundation.

Taasisi inatoa Rai kwa makampuni pamoja na watu binafsi kuendelea kuwasaidia watu wenye uhitaji hususa katika kipindi hiki ambacho tunapambana na mlipuko wa maambukizi ya Covid-19.

C70D-4660C70D-4648